Ezekiel 27:3-8

3 aUmwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ee Tiro, wewe umesema,
“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

4 bMipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,
wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

5 cWalizifanya mbao zako zote
kwa misunobari itokayo Seniri;
Yaani Hermoni.

walichukua mierezi kutoka Lebanoni
kukutengenezea mlingoti.

6 eWalichukua mialoni toka Bashani
wakakutengenezea makasia yako;
kwa miti ya msanduku
kutoka pwani ya Kitimu
wakatengeneza sitaha
Yaani sakafu ya merikebu au mashua.
yako
na kuipamba kwa pembe za ndovu.

7 gKitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,
nacho kilikuwa bendera yako;
chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau
kutoka visiwa vya Al-Yasa.

8 hWatu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;
watu wako wenye ustadi, ee Tiro,
walikuwa ndio mabaharia wako.
Copyright information for SwhKC